Jeremiah 50:7-12


7 aYeyote aliyewakuta aliwala;
adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia,
kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi,
Bwana, aliye tumaini la baba zao.’


8 b“Kimbieni kutoka Babeli;
ondokeni katika nchi ya Wakaldayo
tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.

9 cKwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli
muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini.
Watashika nafasi zao dhidi yake,
naye kutokea kaskazini atatekwa.
Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari,
ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.

10 Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara;
wote wamtekao nyara watapata za kutosha,”
asema Bwana.


11 d“Kwa sababu hushangilia na kufurahi,
wewe utekaye urithi wangu,
kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka,
na kulia kama farasi dume,

12 emama yako ataaibika mno,
yeye aliyekuzaa atatahayari.
Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote,
atakuwa nyika, nchi kame na jangwa.
Copyright information for SwhKC